December 25, 2020

 


BAADA ya kupoteza mchezo uliochezwa Desemba 23 wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum,  kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kutua ardhi ya Bongo.

Simba ilikamilisha dakika 90 kwa kufungwa bao 1-0 ambalo lilipachikwa dakika ya 17 na Perfect Chikwende kwa jitihada binafsi baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Wekundu  Msimbazi. 

Mchezo wa marudio utakuwa Januari 6, 2021 na Simba inatakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili ili kutinga hatua ya makundi.


Kocha Mkuu wa Simba,  Sven Vandenbroeck amesema kuwa watajitahidi kuongeza umakini ili kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.


Jumapili, Desemba 27 ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Majimaji FC mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya tatu.

1 COMMENTS:

  1. Mashindano ya kombe la shirikisho imeanza na upendeleo kwa timu kupewa poinyi tatu za bure!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic