December 10, 2020


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa suala la mchezaji wao wa zamani ndani ya timu hiyo Shiza Kichuya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa, (FIFA) pamoja na wao kutakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani 130,000( M.300) bado hazijafika mezani kwao.


Habari zinaeleza kwamba Kichuya aliyesajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo msimu wa 2019/20 kwa dili la miezi sita bado alikuwa ni mali ya timu yake ya zamani ya Pharco ya Misri ambayo iliinasa saini ya nyota huyo kutoka Simba msimu wa 2018/19.


Nyota huyo alikuwa ameshitakiwa na Klabu ya Pharco ya Misri iliyoinasa saini yake msimu wa 2019 kutokana na madai ya kukatisha mkataba wake ndani ya timu hiyo kisha akajiunga na Simba Januari, mwaka huu.


Shauri hilo lilikuwa linafanyiwa uchunguzi na Kamati maalumu ya DR Congo iliyo chini ya FIFA kabla ya kutoka kwa maamuzi ya faini hiyo ya Kichuya kufungiwa.


Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda amesema:"Taarifa hizo bado ni mpya kwetu, Bodi ya Wakurugenzi hatujapokea taarifa rasmi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wetu, Barbara Gonzalez, hivyo tunasubiri taarifa rasmi ifikishwe kisha tutakaa kuijadili.


"Ila tunawaomba mashabiki wa Simba wawe watulivu kwa sababu maamuzi kama haya yanafanyika lakini hayamaanishi kuwa yapo sahihi.


"Kuna wakati maamuzi yanaweza kufanyika na yasiwe sahihi na ndiyo maana ipo nafasi ya kuweza kukata rufaa na maamuzi yakabadilishwa baada ya kupitiwa upya, nisingependa kuongea mengi kwa sasa tusubiri Barbara atalitolea ufafanuzi," amesema.

Kwa sasa Kichuya anacheza ndani ya Namungo ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara ikiwa chini Kocha Mkuu, Hemed Morroco.


Chanzo:Spoti Xtra

16 COMMENTS:

  1. Unakata rufaa kwenda wapi kama fifa wameamua hill. Machen kuwapumbaza mashabiki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ungenyamaza kama hujui kuna mahakama ya michezo cas unaweza kukata rufaa kama hukubaliani na maamuzi ya FIFA

      Delete
    2. Ni kweli Rodrick, kama jambo hulijui...ni bora usilizungumzie. Vilabu vingi vya soka duniani na pia wanamichezo wengine kwa ujumla wanaitumia sana CAS.

      Delete
  2. Hata maamuzi ya FIFA yaweza kukatiwa rufaa, ni katika Court of Arbitration for Sport (CAS). Hapo sasa ndio mwisho!

    ReplyDelete
  3. Ukirejea Email iluyotumwa Namungo, uamuzi huu wa fine ya Dola 130,000, umetolewa na CAS. Ukiwahusu Simba, Kuchuya kutocheza kwa miezi 6 na Namungo kutomtumia hadi adhabu yake ilipwe.
    Kisichowazi ni hatma ya michezo aliyoshiriki Kichuya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi ninyi watu was Simba akili zenu na huyo anayenukuliwa kuongea zinatia huruma kwa taarifa yenu Kama huyo mchezaji angetoka Timu ya ndani TFF wangechezesha mtambo mala ungesikia usajili wa awali mkataba unatofautiana na ::::; ili mradi kusafisha usanii wa Simba ,refer Morrison Case,hogopa Timu inasajili asilimia 90 kwa kuchungulia wachezaji walomaliza mikataba .HILO MNALO hakuna Cha CAS Wala CUF Wala Nini punguzeni utoto wa mjini .

      Delete
  4. Mkataba si upo na kucheza si alicheza... kukata rufaa ni kuijongezea gharama tu. FIFA sio fff.

    ReplyDelete
  5. Hapa tungeshauri pointi zote Simba ilizopata wakiwa na huyo mchezaji wangenyanganywa kuwapa adabu ,hii haina tofauti na mechi fixing

    ReplyDelete
  6. kichuya anapaswa kuwajibika kwa kusaini mkata na timuu nyingne huku akijua anamkataba na timu nyngne.

    ReplyDelete
  7. Unaweza kukata rufaa kama una uhakika na jambo unalolikatia rufaa,lakini kama huna uhakika ni kupoteza muda na kujitafutia matatizo makubwa zaidi.Kumbuka simba wamepewa siku 45 tu wawe wamelipa kiasi hicho cha pesa,vinginevyo watafungiwa kusajili wachezaji wapya kwa kipindi cha misimu miwili,sasa hapo ndo unapoweza kuona athari ya kukata rufaa pale utakaposhindwa kesi......nyie neng'enekeni tu na kujiongopea........hilo ni trela tu jiandaeni na picha kamili kwenye issue ya morrison.

    ReplyDelete
  8. Simba hawajakataa faini ila wamesema haijawafikia taarifa ya wao kulipa pesa mbona hamuelewi nyinyi utopolo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe mkia ndo huelewi na unapitwa na wakati,kabla ya hiyo taarifa ya simba unayoisema wewe walishasema kuwa watakaa kuona kama wanaweza kukata rufaa,.soma taarifa za jana.

      Delete
  9. Wamesha Umia, hapo maamuzi yametolewa kwa uweledi mkubwa sio TFF wazee wa mbeleko, Kateni rufaa mzidi kukiwa,
    ndio mjifunze sio deal kuzoazoa wachezaji ovyo...!

    ReplyDelete
  10. Pamoja na kutotumika, lkn Hiyo tafsiri yake thamani ya Kichuya ni zaidi ya 300M,
    Hasara ya kiwango cha lami

    ReplyDelete
  11. Ugumu wa hii, kuwa kipindi tunalopoka ugolo wetu huu, kumbuka Kichuya alikaa nyumbani zaidi ya miezi sita

    ReplyDelete
  12. Yaani waandishi.wangetuletea mchanganuo,tupige hesabu wenyewe,ingekua poa sana.lkn tunajadili hukunu na hatujui mwenendo na hoja kesi.basi ni kutomboka tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic