December 31, 2020


 SALUM Kimenya, beki wa Klabu ya Tanzania Prisons amesema kuwa wanahitaji kuvunja rekodi ya Yanga kumaliza mzunguko wa kwanza bila kufungwa kwa kusepa na pointi tatu watakapokutana.

Prisons ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 imekusanya pointi 21 inakutana na Yanga ambayo imecheza mechi 17 ambazo ni dakika 1,530 bila kupoteza ikiwa na sare nne.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa wanatambua kwamba wapinzani wao hawajapoteza hivyo wapo tayari kutibua rekodi hiyo.

“Tunajua kwamba hawajapoteza hilo lipo wazi ila nasi pia tunahitaji pointi tatu kwa kuwa nafasi ambayo tupo kwa sasa sio nzuri.

"Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunahitaji kupata matokeo," amesema.


Mchezo wa leo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nelson Mandela saa 10:00 jioni.


Walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga iligawana pointi mojamoja na Prisons kwa kufungana bao 1-1.

3 COMMENTS:

  1. Mpambane muwafunge hao kandambili bao 2 bila mnaweza mpambane afe beki afe kipa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic