December 31, 2020


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum kila kitu kipo sawa kwa upande wa maandalizi huku wakiwa wameomba kupewa kibali cha kuongeza idadi ya mashabiki.

Mara amesema Klabu ya Simba, imeliomba Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuwaongezea idadi ya watu kutoka 50% ya mashabiki kuingia uwanjani katika mechi dhidi ya Platinum ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa Januari 6, 2021, Uwanja wa Mkapa.


Katika mechi dhidi ya Plateau, Caf iliwapa Simba nafasi ya kuingiza mashabiki 50% ya uwezo wa Uwanja wa Mkapa kwa hofu ya ugonjwa wa Covid 19.

Manara amesema kuwa wanataka zaidi ya idadi hiyo kutokana na hali ya Tanzania kiusalama wa afya ilivyo jambo ambalo limewafanya watume maombi ya kupewa kibali cha uongezeko la mashabiki zaidi.


Pia ameongeza kuwa kutakuwa na punguzo la viingilio ndani ya uwanja ambapo awali ilipangwa kuwa 7,000 ila sasa itakuwa 5,000 mzunguko VIP B na C ilipangwa iwe 20,000 lakini sasa itakuwa 15,000.

Lakini mashabiki wanatakiwa kupata tiketi kabla ya Jumatatu ikiwa watahitaji kununua siku ya mchezo basi watakuwa na kazi ya kununua tiketi kwa bei ile ya awali.

Kwenye mchezo huo Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwa kuwa ilipoteza mchezo wa kwanza nchini Zimbabwe kwa kufungwa bao 1-0.

Inatakiwa kufanya jambo moja pekee, kushinda zaidi ya mabao mawili huku ikilinda lango lake lisitikiswe ndani ya dakika 90.

4 COMMENTS:

  1. Mwenyezimungu atatujaalia inshaalah tutashinda 3 inshaalah

    ReplyDelete
  2. Kwanza ile ya plateau mlifka hata robo ya uwanja

    ReplyDelete
  3. kwan mlipowafunga plateu kwao mlijaza uwanja ?
    manara acha kujipa presha

    ReplyDelete
  4. Tunataka mapato ya uwanjani na ushindi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic