December 14, 2020


KHELFFIN Salum Hamdoun, nyota wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Saudi Arabia baada ya kuvunjika kidole akiwa mazoezini. 

Saudi Arabia imeomba mechi ya marudiano na Ngorongoro Heroes baada ya ule wa kwanza uliochezwa hivi karibuni kushuhudia ikimaliza dakika 90 ikiwa imefungwa bao 1-0.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo, 'Julio' amesema kuwa ni mchezaji mmoja ambaye atakosekana kwenye mchezo wa leo.

"Fini ameumia kidole alipokuwa mazoezini hivyo ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Saudi Arabia ambao ni wa marudio.

"Aliumia wakati akigombea mpira na mwenzake kwenye mazoezi hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza lakini anaendelea vizuri," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic