December 23, 2020

 


LEO ni leo wahenga walisema kwa kwamba mbivu na mbichi zitajulikana kwa wawakilishi wetu wa kimataifa kujua mwanzo wa kule ambako wanahitaji kuelekea.

Kufanya kwao vizuri kwenye mechi za mwanzo ni hatua nzuri na itawaongezea nguvu ya kupambana kwenye mechi zijazo kwa sababu watakuwa wamepata sehemu ya kuendelea pale ambapo walikuwa wameishia.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wapo nchini Zimbabwe na watakuwa na kazi ya kufanya mbele ya FC Platinum.

Wasirudie makosa ambayo waliyafanya kwenye mchezo dhidi ya UD Songo msimu uliopita kwa kuwa walishindwa kufika mbali baada ya kukosa matokeo ugenini na nyumbani kulazimisha sare.

Kukumbuka makosa waliyoyafanya msimu uliopita sio suluhisho la matatizo bali wanatakiwa wayakumbuke na kuyafanyia kazi.

Maisha yanakwenda kasi na kila siku mbinu zinabadilika. Ni wakati mwingine wa kufanya vizuri ugenini ili kupunguza presha kwenye mchezo wa marudio.

Timu imeshawasili Zimbabwe tena iliweka kambi mapema kabisa. Hili kiufundi ni faida kwa wapinzani kuweza kuzitambua mbinu zenu nanyi pia mmmepata faida ya kuyazoea mazingira.

Kwa kuwa mbinu zenu wakati huu zipo mikononi mwa wapinzani wenu basi fanyeni kazi ya ziada kusaka ushindi ugenini.

Ulimwengu wa mpira kwa sasa mambo yamebadilika na kila mmoja ana nafasi ya kushinda ugenini kwa namna yoyote ile.

Jambo la msingi ni kuongeza juhudi na kufanya mbinu mpya ambazo zitawapa matokeo. Imani yangu ni kwamba wachezaji wanatambua uzuri wa mashindano ya kimataifa.

Mbali na wachezaji hata benchi la ufundi pia linatambua umuhimu wa mashindano ya kimataifa. Hapa ni sehemu pekee inayowaweka wachezaji kwenye ramani pamoja na benchi la ufundi kwenye kuongeza CV.

Ugenini kuna kazi kusaka ushindi ila inawezekana ikiwa kutakuwa na nia na makubaliano ya pamoja. Ni wakati mwingine ambao tunaamini kwamba wachezaji mtapeperusha bendera na kupata matokeo chanya.

Namungo pia ni wawakilishi wetu kwenye Kombe la Shirikisho hawa watavaana na El Hilal Obeid.Hawa watakuwa nyumbani kwenye mchezo wao huu muhimu.

 Tunaamini kwamba kazi ya nyumbani itakuwa ni kusaka ushindi kwenye mchezo huu sapoti ya mashabiki itakuwa nanyi Namungo kazi ni kwenye kupambana ndani ya uwanja.



Leo macho na maskio ya mashabiki ni kwenu ninyi wawakilishi wetu. Msifanye makosa kwenye mechi hizi ambazo ushindani wake ni mkubwa.

Pia mkipata matokeo msibweteke na kuanza kujilinda ilihali kuna muda wa kufanya vizuri kupata matokeo zaidi.Ikiwa itakuwa ni kwa tabu sana anzeni kutafuta ushindi wa mabao matatu na kuendelea ili kushusha presha.

Kwa watakaoanza nyumbani wana nafasi kubwa ya kupata matokeo na wale watakaokuwa ugenini nao wana nafasi ya kufanya vizuri kwa sababu mpira ni kitu cha wazi na dakika 90 zitazungumza.

Kwa namna ambavyo mtaanza kwenye mashindano haya leo mkiwa hatua nyingine mtafikia malengo ambayo mmejiwekea. Na ushindi wenu ni kwa ajili ya taifa kiujumla sio timu pekee.

Ukweli ni kwamba wachezaji mmeshikilia dhamana na furaha ya mashabiki pamoja na wale ambao wanawafuatilia kila saa kila wakati.

Kazi iwe moja ndani ya uwanja kwa wachezaji kusaka ushindi kwa namna yoyote.Kila kitu kinawezekana na ushindi upo mikononi mwenu.

Simba na Namungo mpo kazini leo msisahau kwamba ushindi wenu ni kwa ajili ya taifa hivyo msijisahau mkiamini kwamba mtafanya vizuri kwenye mchezo wa marudio.

Mchezo wa marudio kila timu huwa inakuwa na mbinu zake kwa sababu ninyi mnaanza leo basi vurugeni mbinu za wapinzani wenu kabla hawajarudi kuwavaa kwenye mechi za marudio.

Kazi ni kwenu wachezaji kucheza kwa juhudi ndani ya uwanja kusaka ushindi kwa kila namna.Yote yanawezekana na kila kitu kinawezekana.

Watanzania na mashabiki ni wajibu wetu kuwapa sapoti ndugu zetu na kuongeza dua ili waweze kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Imani yetu ni kwamba hamtawaangusha Watanzania bali mtafanya vema katika kazi zenu na kuongeza ushindani kwenye mechi za marudio ambapo kazi yenu ya kwanza mtakuwa mmeikamilisha kwa umakini mkubwa.

1 COMMENTS:

  1. Maelezo mengi muda wa mchezo hausemwi. Waandishi wetu mnakwama wapi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic