UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetoa shukrani kwa mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi kuipa sapoti kwenye mchezo wao wa jana Desemba 12 dhidi ya Mwadui FC.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Yanga inayonolewa na Cedric Kaze iliweza kupata ushindi wa mabao zaidi ya matatu kwenye mchezo mmoja.
Mara ya mwisho kwa msimu wa 2020/21 Yanga kupata ushindi mkubwa ilikuwa ni dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa iliposhinda mabao 3-0.
Ilishinda jumla ya mabao 5-0 jana ukiwa ni ushindi mkubwa kwa msimu wa 2020/21 ambapo imecheza jumla ya mechi 15 bila kupoteza ikiwa nafasi ya kwanza.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema shukran kwa mashabiki kwa sapoti kubwa na waendelee kuwapa sapoti bila kuchoka.
Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi 37 huku inafuatiwa na Simba yenye pointi 29 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 13.
Kila la kheri
ReplyDeleteForever young
ReplyDelete