December 13, 2020

 



UWANJA wa Sokoine dakika 90 zimekamilika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Inasepa na pointi tatu na kufikisha pointi 29 n kushusha Azam FC nafasi ya pili 
Zinaongezwa dk 2
Dakika ya 90 Mbeya City wanamchezea faulo Chama, inaanzisha faulo na Tshabalala 
Dakika ya 88 Kibu anatoka anaingia rasta Chidebele
Dakika ya 81 Nyoni ndani anatoka Said Ndemla 
Dakika ya 73 Sheva ndani Dilunga anatoka
Dakika ya 71 Onyango anaokoa hatari ndani ya 18 baada ya Kibu Denis kuingia na mpira ndani ya 18 ila mwamuzi wa pembeni alikuwa amenyayua kibendera
Dakika ya 70 Chama anapeleka kwa Ndemla, Mkude,Onyango,Ndemla,Chama,Mkude kuelekea lango la Mbeya City 
Dakika ya 66 Mpoki anapewa huduma ya Kwanza na Meddie Kagere pia baada ya purukushani za hapa na pale
Dakika ya 63 Mbeya City wanapata faulo nje kidogo ya 18 inaokolewa na Manula
Dakika ya 62, Kagere anaotea
Dakika ya 57 Kapombe anacheza faulo kwa nyota wa Mbeya City 
Dakika ya 55 Kibu anachezewa faulo na Ame ambaye anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 54 Kipa wa Mbeya City anaokoa hatari 
Dakika ya 45 John Bocco anatoka anaingia Mugalu
Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Sokoine 
Mapumziko: Yanga 0-1 Simba

Dakika ya 45+2 Said Ndemla anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika 2 zimeongezwa
Dakika ya 44 Denis Kibu anapiga kichwa ndani ya 18 kinakwenda nje kidogo ya lango la Manula
Dakika ya 41 Ndemla anafanya jaribio nje ya 18 linakwenda juu ya lango
Dakika ya 33 Goooooal John Bocco
Dakika 30 Mbeya City wanaanua majalo
Dakika ya 28 Mbeya City wanapiga kona moja sawa na Simba zote hazijawa na faida
Dakika ya 22 Chama anapiga faulo haizai matunda inaanuliwa na mabeki.
Dakika ya 21 Mpoki Mwakinyuke anaonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 20 kipa wa Mbeya City Lamek anaokoa hatari ndani ya 18
KIPINDI cha Kwanza Uwanja wa Sokoine 


Mbeya City 0-0 Simba


Dakika  15 za mwanzo zimekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu ndani ya Uwanja wa Sokoine. 

8 COMMENTS:

  1. Mwandishi amka, acha kuota yanga. Leo simba inacheza ma mbeya city sio yanga, sasa unapoandika mapumziko, yanga 0 simba 1 unataka kuua watu kwa presha?

    ReplyDelete
  2. Yan hii blog bhn,, kwamba HT yanga 0 -1 simba?? Kwahyo leo n yanga na simba na cyo mbeya city na simba?? Haaa haaa

    ReplyDelete
  3. Hi nayo kali sasa uto sijui wanajisikieje????

    ReplyDelete
  4. Huyu Saleh naye! Yanga 0 simba 1 imetoka wapi mechi ya Mbeya city na Simba?

    ReplyDelete
  5. Blog hii haiko makini mnaandika bila weledi wowote. Tasnia ya habari inahitaji kuweka ushabiki pembeni. Umakini ni muhimu

    ReplyDelete
  6. Kifo cha tasnia ya habari kimewadia iliyobaki ni mazishi tu.
    Usije shangaa mwisho wa mchezo akaandika "Full time" Platinum 0 Simba 2

    ReplyDelete
  7. Yupo sawa kabisa simba leo alikuwa anacheza na Yanga kwani yanga aliekeza nguvu zote kwa mbeya city amfunge simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic