WAKALA wa kiungo mshambuliaji raia wa Burundi, Erick Kwizera 'Messi' anayefahamika kama Nkurahija Bonheur amefunguka kuwa anaamini Namungo ndiyo sehemu sahihi kwa ajili ya kukuza kiwango cha mteja wake.
Kwizera amejiunga na Namungo kwenye usajili wa dirisha dogo lililofungwa Januari 15, mwaka huu ambapo tayari amejumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.
Straika huyo tayari ameifungia Namungo mabao mawili tangu ajiunge na kikosi hicho.
Akizungumzia dili la Kwizera Nkurahija amesema: "Naamini Namungo ni mahala sahihi kwa mchezaji wangu na ndiyo maana yupo pale licha ya hapo awali kupokea ofa nyingi sana baada ya kuonekana kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kule Zanzibar.
"Najua malengo yake na ndiyo maana nilimpeleka pale kwa kuwa nina uhakika kuwa Namungo watamfikisha pale anapotaka kufika kwenye soka,"
0 COMMENTS:
Post a Comment