January 21, 2021

 



MLINDA mlango mpya wa klabu ya Azam, Mathias Kigonya amefunguka kuwa malengo yake ni kuhakikisha anacheza kwa kiwango kikubwa, ili kuliweka salama lango la klabu hiyo dhidi ya washambuliaji hatari kama Meddie Kagere.

Kigonya alikamilisha rasmi usajili wa kujiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili Januari 14, mwaka huu akitokea kwenye kikosi cha klabu ya Forest Rangers ya Zambia ambapo akiwa na kikosi hicho alifanikiwa kuibuka na tuzo ya mlinda mlango bora kwa misimu miwili mfululizo iliyopita.

Kigonya akiwa na Rangers msimu uliopita alifanikiwa kusimama langoni kwenye michezo 14 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa yaani ‘Cleen Sheet’ kati ya michezo 23.

Akizungumzia malengo yake ndani ya kikosi cha Azam Kigonya amesema: “Nimefurahi kutua ndani ya kikosi cha klabu ya Azam, najua ligi ya Tanzania ni ngumu na ina washambuliaji bora lakini naamini kupitia uwezo wangu nitapambana kuliweka salama goli la Azam dhidi ya washambuliaji wasumbufu kama Kagere ambaye najua amekuwa mfungaji bora mara mbili hapa,”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic