January 22, 2021

 


UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema licha ya jina la kiungo mkabaji raia wa Uganda, Taddeo Lwanga kutokuwemo kwenye orodha iliyopelekwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), bado mchezaji huyo ni mali yao.

Jina la Lwanga halipo kwenye orodha ya majina yaliyopelekwa (TFF), na Simba kama sehemu ya usajili wao wa dirisha dogo wa wachezaji watakaotumika kwenye mzunguko wa pili wa ligi, hali ambayo ilizua maswali mengi kwa wadau wa soka.

Nyota huyo aliyetambulishwa rasmi na Simba Desemba 2,2020 amepata nafasi ya kuichezea Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Alishuhudia Kombe la Mapinduzi likienda kwa watani zao wa jadi Yanga baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 kwenye fainali kwa kuwa dakika 90 ngoma ilikuwa sare ya bila kufungana.  

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema: "Yamekuwepo maneno mengi kuhusu mchezaji wetu Taddeo Lwanga kutokana na ukweli kwamba jina lake limekosekana katika orodha iliyoenda TFF.

"Lakini niwatoe hofu kwani Lwanga bado ni mchezaji halali wa Simba na kuhusu kinachoendelea tusubiri siku ya utambulisho wa wachezaji kwenye michuano ya Simba Super Cup na wote tutajua," .

4 COMMENTS:

  1. Kwa maana hiyo CEO Boss Lady anatujulisha kuwa Lwanga atasubir hadi msimu ujao au vipi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. KUNA UWEZEKANO WAKUWA NI MCHEZAJI WA SIMBA SIKU ZOTE KAMA MKATABA WAKE HAUJAVUNJWA, MAANA HATA BARCA WANA WACHEZAJI LUKUKI NJE YA KIKOSI CHA LIGI NA UEFA CHAMPION LIGUE.

      Delete
  2. Huyu kwakweli aende tuu, galasa huyu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic