UNAAMBIWA usiulize kuhusu mshahara wa mshambuliaji mpya wa Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak, kwani walichokifanya Yanga kwa mshambuliaji huyo ni kufuru.
Taarifa za ndani ya Yanga zinaeleza kuwa straika huyo amepewa mkataba utakaomfanya alipwe kiasi cha dola za Kimarekani 9500 sawa na fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 22 kwa mwezi.
Tayari Yanga imeshatangaza kumsajili Fiston ambaye ni raia wa Burundi aliyekuwa akiitumikia Klabu ya Enppi ya nchini Misri.
Mtoa taarifa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema: "Taarifa sahihi juu ya usajili wa Fiston mimi najua wazi kuwa hadi tunamalizana naye tulikubaliana kumlipa mshahara wa dola 9500, kwa kila mwezi,"
Huyo kiongozi hafai, mshahara ni siri kati ya walioingia makubaliano
ReplyDeleteHaki ya Mungu Kama ni kweli tusubiri tumuone uwanjani pia tatizo la kutowekeza kwa wazawa timu ya taifa inapwaya maana tunashindwa kuandaa wazawa hiyo hela tunawalipa wageni
ReplyDeleteUnione wivu, na wachezaji wetu wanayo nafasi ya kwenda nje, wapigieni debe waende, na wenyewe watalipwa vizuri
Delete