KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Klabu ya Simba kinatarajiwa kurejea rasmi kambini Januari 25, ambayo ni siku ya Jumatatu ya wiki ijayo.
Tangu kumalizika kwa michuano ya Kombe la
Mapinduzi, kikosi cha Simba kilipoteza fainali ya michuano hiyo mbele ya Yanga
kimekuwa kwenye mapumziko.
Inatajwa kuwa siku hiyo Simba inaweza kuanza
rasmi mazoezi na kocha wake mpya ambaye yuko kwenye mchakato wa kutangazwa hivi
karibuni, ili kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara pamoja na ile ya Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Simba inatarajiwa kuanza kibarua chake kwenye
Ligi ya mabingwa Afrika Februari 12, mwaka huu dhidi ya AS Vita kutoka DR
Congo.
0 COMMENTS:
Post a Comment