January 19, 2021

 


JUVENTUS inajipanga kumsajili kiungo wa Manchester United,  Paul Pogba mwenye miaka 27 katika usajili ujao wa majira ya joto.

Mabosi wake wa zamani Juventus wanaamini kwamba United itapunguza dau la Mfaransa huyo ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2022.

Akiwa chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksjaer kwa sasa ameanza kuaminika na kupewa namba kikosi cha kwanza jambo ambalo linaongeza ugumu kwa mabosi wa timu hiyo kuweza kumpa ruhusu ya kusepa.

Licha ya kwamba awali Pogba alikuwa anasema kuwa anahitaji kupata changamoto mpya kwa sasa ameonekana kuwa na furaha ndani ya kikosi hicho.

Wakati United ikilazimisha sare ya bila kufungana na Liverpool, Uwanja wa Anfield, Pogba alianza kikosi cha kwanza ana alifanya vizuri uwanjani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic