NYOTA wa Klabu ya Namungo, Stephen Sey raia wa Ghana amesema kuwa malengo yake ni kuwa mfungaji bora ndani ya Kombe la Shirikisho ambalo timu hiyo inashiriki.
Sey ambaye yupo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morroco ametupia jumla ya mabao manne kwenye Kombe la Shirikisho na timu yake imetinga hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho.
Ikiwa ipo hatua ya 32 bora ina kazi ya kupambana na CD de Agosto ya Angola kwa ajili ya kufuzu hatua ya makundi mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa Februari.
Nyota huyo amesema:"Ninaona kwamba timu inafanya vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kufanya vizuri kitaifa na kimataifa jambo ambalo linaongeza nguvu kwangu nami kufanya vizuri.
"Ninahitaji kuwa mfungaji bora ndani ya Kombe la Shirikisho kwa ajili ya manufaa ya timu yangu na taifa kiujumla hivyo nitapambana ili kuwa bora zaidi na zaidi," .
0 COMMENTS:
Post a Comment