January 31, 2021


 HARRY Kane, mshambuliaji wa kikosi cha Tottenham imeelezwa kuwa anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu tofauti na ilivyoelezwa awali.

Kane aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool uliochezwa Alhamisi iliyopita ambapo timu yake ilifungwa mabao 3-1.

Taarifa zimekuwa zikisema kuwa mchezaji huyo anaweza kukosa mchezo wa timu ya Taifa ya England wa kufuzu Kombe la Dunia unaotarajiwa kuchezwa Machi mwaka huu 2021.

Kocha Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa ni kweli mchezaji wake ameumia ila muda ambao atakaa nje ya uwanja bado hajatambua.

"Kweli Kane ameumia ila kuhusu majeraha yake na muda ambao atakosekana ni jambo ambalo linahitaji muda hivyo tusubiri na tuone," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic