January 15, 2021

 




KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa kikosi cha Simba hakina uwezo wa kuwa na makali ndani ya uwanja ikiwa mchezaji wao Clatous Chama hatakuwepo.

Yanga ilishinda kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi mbele ya Simba kwa ushindi wa penalti 4-3 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan Januari 13.

Ndani ya dakika 90 wababe hao walitoshana nguvu bila kufungana na kupelekea kufikia hatua ya matuta ambayo yaliamua nani awe bingwa.

Kwenye kikosi cha Simba hakuwepo Chama ambaye alikuwa amepewa mapumziko na mabosi wake kutokana na kutumia nguvu nyingi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.



Kaze amesema:"Naona kwamba Simba ni timu nzuri ila inakuwa haina yale makali ambayo yamezoeleka ikiwa hakutakuwa na mchezaji Chama(Clatous).

"Yeye amekuwa akiamua namna ya kucheza na kupeleka mashambulizi, pia ana akili ya kuleta hatari muda wowte hivyo ninaamini kwamba Simba ni timu nzuri ila ikiwa haina Chama inakuwa haina hatari sana ndani ya uwanja," .

Yanga imetwaa taji lake la pili la Kombe la Mapinduzi na zawadi ya shilingi milioni 15 huku Simba wakiwa ni washindi wa pili na zawadi yao ni shilingi milioni 15.

8 COMMENTS:

  1. Bora unaamini nintimu nzuri mengine waachie wenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaze uwaulize pia viongozi wa Yanga hasa Nugaz Ten na Bumbuli ile ahadi na kujiaminisha kuhusu usajili wa Chama Yanga umefikia wapi na hili ni dirisha dogo.

      Delete
  2. Ila nitawashangaa viongozi wa simba wakiendelea kutia masikio yao pamba kuhusu suala hili la simba bila ya chama ni bure kabisa.Chama huyu alishawahi kudhibitiwa mara kadhaa na simba kutaabika sana ama kupoteza ushindi. Ila hakujawa bado na mpango mkakati wa mtu wa kumreplace chama inapotokea hali kama hiyo.kwanza simba ina tatizo la straika mwenye uwezo au ujasiri wa kwenda kuwakera mabeki wa timu pinzani.Fowadi ya simba yote ni ya kukimbia mabeki wabeki hata Lusajo wa KMC ni wa tofauti kidogo.

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo kocha anakiri kuwa Chama angekuwapo timu yake ingefungwa?

    ReplyDelete
  4. Kocha kwenye weledi hawezi kutoa kauli kama hiyo,kwa mantiki hiyo Yanga bila Saido haipati ushindi. Huko ni kukosa weledi mbona mechi ya kwanza Chama alikuwapo na Simba haikushida. Aache mashabiki waongee na yeye afanye kazi iliyomleta

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo kukosa weledi tu bali ni kukosa kumbukumbu. Simba walizifunga Chipukixi, Mtibwa na Namungo. Simba hawakuwa na mechi waliyotoka sare hata moja. Chama alikuwepo? Huyu kocha aangalie uwezo wa wachezaji wa Yanga aliyokiri alihusika kuwasajili mfano Sarpong na Carlinhos

      Delete
  5. Hivi yanga ndiyo timu iliyokamilika? Wamefunga magoli mangapi mpaka mashindano yanaisha? Au ndiyo kusema bila hirizi ya Shikhalo hakuna timu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shikhalo alimtuma mjumbe kwenda kumchukulia "mzigo" wake aliokuwa ameusahau golini. Daah!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic