January 21, 2021

 



KUFUATIA kuikatia rufaa kamati ya uchaguzi ya Klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Boniface Lihamwike kwa muda wa siku 20 sasa, kupinga jina lake kukatwa katika kinyangan’yilo cha kuwania uenyekiti, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekuita Hassan Dalali ili kuweza kuanza mchakato wa kusikiliza rufaa yake hiyo. 

Dalali aliikatia rufaa kamati ya uchaguzi ya Simba kwenda TFF kupinga kukatwa jina lake katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa klabu hiyo unaotarajia kufanyika Februari 7 kufuatia aliyekuwa mwenyekiti wa nafasi hiyo, Swed Mkwabi kujiuzuru Septemba mwaka juzi kutokana na sababu zake binafsi.

Aidha kamati hiyo tayari imeshafungua kampeni iliyoanza Jumapili iliyopitan huku ikiwa inadumu dani ya siku 21 ikiw ana wagombea wawili Juma Nkamia na Mutaza Mangungu huku watatu kati yao Hamisi Omari Tika, Rashid  Shangazi na Anton Mwakisu wakijitoa dakika za mwisho. 

Akizungumzia wito huo Dalali amesema: “TFF wameshaniita kupitia kwa katibu mkuu Kidau ambaye alinipigia simu na kunitaka niwasilishe kopi ya rufaa yangu na tayari nimeshafanya hivyo na ameshanieleza ndani ya wiki hii inaweza kusikilizwa,” 

4 COMMENTS:

  1. Mzee usilazimishe elimu ndio muhimu zaidi hii simba sio ile ya enzi zenu mzee wangu

    ReplyDelete
  2. Hawa ndio walianzisha Simva day na kununua uwanja wa bunju wakati wasomi wenu hawakufanya xhochote

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hajui kuwa hao wasio na elimu ndo waliojenga jengo la klabu na kuiendesha timu kwa hela za kutoka mifukoni mwao.Wazaramo wana msemo wao "Kusoma sio kwisha ujinga"

      Delete
  3. Elimu ni maaarifa, sio lazima mtu awe na cheti, angalia wasomi wangapi wamesajiliwa na wasiokua na vyeti, chukua mfano mdogo tu mafanikio ya Wasafi Media CEO wake anaelimu kiasi gani?
    Maaarifa ndio jambo la msingi lkn elimu ya vyeti isikudanganye, watu wengi wanakariri kwaajili ya mtihani lkn hawana maaarifa ya walichosomea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic