IMEFAHAMIKA kwamba, mabosi wa Yanga wamekubaliana kumbakisha mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kwa masharti mazito yatakayomfanya aendelee kudumu katika kikosi hicho.
Sarpong aliyejiunga na Yanga msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili, ameonekana kutokuwa na kiwango bora cha mwendelezo kiasi cha kufikiriwa jina lake kukatwa.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Sarpong amepewa sharti la kufunga mabao zaidi ya kumi msimu huu, huku hivi sasa akiwa tayari amepachika manne katika ligi.
Mtoa taarifa huyo alisema kama mshambuliaji huyo atashindwa kufikisha idadi hiyo ya mabao, basi watausitisha mkataba wake.
“Yanga ilikuwa ina matarajio makubwa na Sarpong katika msimu huu ikiwemo kufunga mabao, lakini ameonekana kushindwa kuonesha ubora wake.“
Hivyo, uongozi ulifanya naye kikao na kukubaliana baadhi ya vitu kati ya hivyo ni kumpa sharti la kufunga mabao zaidi ya kumi ili aendelee kubaki ndani ya Yanga kwa msimu mwingine,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa kuzungumzia hilo, alisema: “Ishu ya Sarpong hivi sasa amerudi kwao Ghana kwa ruhusa maalum ya uongozi, atarudi kambini Januari 25, mwaka huu.”
jaman si watafanya yanga isifunge maana akiwa nao surpong hatatoa pasi ataangalia kibarua chake kwanza, heeeheee hiii blog ni mwisho
ReplyDeleteWanazidi kumuongezea presha, utakuta yeye na nyavu anakosa
ReplyDeleteSaf Sana uongozi sarpong Bado n mchezaj mzur apewe muda zaid
ReplyDeleteHuo nimzigo bora akaondoka kocha akaendelea kumtumia wazir kuliko sarpong. Sarpong kwa namuona ni Kama yiipe ali chagamuka
ReplyDeleteHuo mzigo sasa kwa saprong je Kama hatatowah assist je
ReplyDeleteAbaki2 ipo siku atatubeba tusipotegemea
ReplyDeleteAbaki2 ipo siku atatubeba tusipotegemea
ReplyDelete