January 30, 2021


CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa Klabu ya KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuzilamba Ice Cream za wapinzani wao Azam FC kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, saa 4:30 jioni leo Januari 30.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Geroge Lwandamina itawakaribisha Wanakino Boys kwenye mchezo wa kirafiki ambao ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya mzunguko wa pili.

Christina amesema kuwa wamejipanga kwa ukamilifu kwenye mchezo wa leo kupata matokeo licha ya kwamba ni mchezo wa kirafiki.

"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC, tunahitaji kulamba Ice Cream na kuonyesha kwamba sisi tunaweza na tupo imara.

"Mbali na kwamba ni mchezo wa kirafiki vijana wetu wapo imara na wataonyesha kwamba ile mwendo wa pira spana, pira kodi inaendelea ndani ya uwanja.

"Utakuwa ni mchezo maalumu kwa ajili ya kuweza kurejea kwenye ubora wetu pale ligi itakapoanza hasa ukizingatia kwamba tunarudi kwenye ligi na tutaanza na mchezo wetu dhidi ya Namungo FC,".

KMC itaanza kumalizana na Namungo FC Februari 4, Uwanja wa Uhuru mchezo wa kiporo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic