January 31, 2021


 TIMU ya Masoko kutoka Kampuni ya Global Group kambao ni wachapishaji wa magazeti namba moja kwa habari za michezo kupitia gazeti la Spoti Xtra imeingia mtaani leo Januari 31 kutoa zawadi kwa wateja wake.

Ziara ya leo ilikuwa ni maeneo ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam ambapo kuna tukio la mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe.

Unatarajiwa kuchezwa mchezo wa mwisho kilele cha mashindano ya Simba Super Cup, ambap wenyeji Simba watamenyana na TP Mazembe.

Mashabiki wa Simba na TP Mazembe wamepata bahati ya kupewa tiketi bure baada ya kupata nakala ya gazeti bora siku ya Jumapili la Spoti Xtra.


Anthon Adam, Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji kutoka Global Publishers amesema kuwa ni kawaida ya kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wasomaji wake ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.


“Hii imekuwa desturi yetu kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono, hivyo ni jambo jema kuwarudishia kile tunachokipata kutoka kwao, kwa kuwa sote ni familia ya SpotiXtra.

 

“Wasomaji wetu tuliowakuta wakiwa na nakala ya gazeti la SpotiXtra tumewapa tiketi ya kuingilia kwenye mechi ya Simba dhidi ya Tp Mazembe, hii imekuwa ni kawaida yetu kuwapa tiketi wasomaji wetu wanaokutwa wakiwa na nakala ya gazeti," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Hapo hakuna mashabiki wa Tzp Mazembe, ni mashabiki wa yanga waliojitoa ufahamu

    ReplyDelete
  2. Hao wamepokea tiketi ya bure sio kuishangilia Simba bali kuishabikia Mazembe kama ilivo ada yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic