MASHINE ya kazi ndani ya Yanga, Saido Ntibanzokiza amesema kuwa atafanya mambo makubwa kikosini hapo ili kutimiza malengo ya timu pamoja na majukumu yake.
Ntibanzokiza alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha kwanza ambacho kilitwaa taji la Mapinduzi, Januari 13.
Penalti yake ya mwisho iliamua Yanga iwe bingwa baada ya kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya kutokuwa na chaguo la kuoka penalti hiyo ya ushindi.
Yanga ilishinda kwa penalti 4-3 ambapo nyota wa mchezo kwenye fainali hiyo alikuwa ni beki kisiki ndani ya Simba, Joash Onyango ambaye alikuwa kwenye ubora wake huku wakipeana tabu na Ntibanzokiza ndani ya dakika 90.
Ntibanzokiza amesema:"Bado kuna mambo mengi ambayo ninapaswa kuyafanya ndani ya Yanga hivyo ahadi yangu kwa mashabiki ni kuweza kuona mambo mengi mazuri.
"Imani yangu ni kwamba kwa kushirikiana na wachezaji wenzagu pamoja na benchi la ufundi kiujumla itafungua milango ya mafanikio,kikubwa sapoti kutoka kwa mashabiki," .
Ndani ya Yanga ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 44 amefunga mabao mawili.
Yeye ni ingizo jipya kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa mchezaji huru ila alikuwa anakipiga timu ya Taifa ya Burundi.
Tabu gani alio wapa simba? Huna cha kuandika? Jiweke ww na picha yako
ReplyDelete