January 19, 2021

 


NYOTA wa kikosi cha Azam FC, Prince Dube raia wa Zimbabwe amesema kuwa anaamini atarejea kwenye ubora wake baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Novemba 25, Dube aliumia mkono kwenye harakàti za kusaka ushindi mbele ya Yanga, Uwanja wa Azam Complex ambapo timu yake ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga lilifungwa na nyota wa kikosi hicho, Deus Kaseke ambaye leo atakuwa na kazi ya kupambania taifa la Tanzania, Taifa Stars kufanya vizuri kwenye mchezo wa Chan, nchini Cameroon kwa kuwa yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania.

Tayari Dube amerejea uwanjani na yupo na timu Visiwani Zanzibar akiendelea kupambana chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina. 

Amecheza mechi mbili za kirafiki ambapo mchezo wa kwanza ilikuwa mbele ya Mlandenge na Azam FC ilishinda mabao 2-0 kisha mchezo wa pili ilikuwa ni dhidi ya KMKM ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Nyota huyo amesema:"Nipo imara na nimerudi kazini, imani yangu ni kuendelea kufunga kila ninapopata nafasi.

"Kazi yangu ni kufunga hasa ninapopata nafasi ikiwa nikakosa basi nina kazi ya kutengeneza nafasi kwa wenzangu ambao ninacheza nao, sisi ni familia na furaha yetu ni ushindi," .

Kesho, Januari 20, Azam FC itamenyana na Zanzibar Combine kwenye mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan.


Ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia mabao sita na ana pasi nne za mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic