January 23, 2021


MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Simba raia wa Nigeria, Junior Lokosa amewasiri rasmi nchini Tanzania leo kwa ajili ya kukamilisha taratibu zake za kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Simba.

Kivutio kikubwa kwenye ujio wa Lokosa aliyepokelewa na Katibu Mkuu wa Simba, Dk. Arnold Kashembe ni wingi wa mabegi aliyokuja nayo ukizua maswali mengi kama amehamia moja kwa moja au vipi, kwani nyota huyo alikuwa na mabegi manne makubwa mawili na ya madogo mawili.

Lokosa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo baada ya Mzimbabwe, Tatenda Perfect Chikwende na Mkongomani Gikanji Doxa na Taddeo Lwanga raia wa Uganda.

Lokosa mwenye umri wa miaka 27 ana uzoefu na soka la Afrika ambapo amewahi kucheza nchini Nigeria na Tunisia katika klabu za Esperance, Kano Pillars na First Bank.




6 COMMENTS:

  1. DAH! MSHAANZA KUMDIS TAYARI KISA KAJA NA MABEGI MENGI. ULITAKA AKIFIKA AKAAZIME VIATU AU AENDE KARUME KUNUNUA NDALA JAMANI? AMEJIANDAA JAMANI KWA KILA KITU

    ReplyDelete
  2. kwani anamkataba wa miezi 6 kama Fistoni au Morrison alivyoanza Yanga...Hakuna mchezaji Simba hupata mkataba chini ya mwaka..vitu vya mwaka ni vingi hivyo na mabegi yanapaswa kuwa mengi

    ReplyDelete
  3. Mwanamme kafika kwa siri kubwa na hata wambeya safari hii hawakujuwa

    ReplyDelete
  4. Mabegi yasiwatishe, labda ni mpenzi wa nguo

    ReplyDelete
  5. Duuh UTOPOLO wameshaanza kuogopa mabegi

    ReplyDelete
  6. Utopolo wanaweweseka mapemaa na bado

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic