KLABU ya Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco imeingia kambi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho huku ikijivunia uwepo wa kiungo wao Eric Kwizera.
Nyota huyo ni usajili mpya kwenye dirisha dogo akiwa amesaini dili la miaka miwili kuhudumu ndani ya timu hiyo.
Namungo inawakilisha nchi kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho ikiwa imetinga hatua ya 32 bora ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya CD 1 de Agosto ya Angola.
Mchezo huo ambao utaamua hatma ya Namungo kutinga hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Februari 14 na wataanzia ugenini kabla ya kurudi kumaliza kete ya mwisho, Dar.
Kidamba Namlia, Ofisa Habari wa Namungo FC amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini watafanya vizuri.
"Usajili wa Kwizera umekamilika na imani yetu ni kwamba atatimiza majukumu yake ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho kwa kuwa benchi la ufundi limekubali uwezo wake," .
Kwizera alionesha ubora wake kwenye Kombe la Mapinduzi na alitupia bao moja huku akikutana na kigongo cha mabingwa watetezi kwa mara ya kwanza Simba akiwa visiwani Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment