ETTIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Zambia.
Leo safari ya Stars kufuzu robo fainali ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa Ligi ya ndani inaanza nchini Cameroon.
Stars imepangwa kundi D ikiwa na timu ya Guinea, Zambia na Namibia ambapo leo chezo wake wa kwanza itakuwa dhidi ya Zambia.
Kwenye kikosi hicho yupo mkongwe mmoja ambaye ni kiraka, Erasto Nyoni ambaye alikuwa ndani ya kikosi kilichoshiriki mashindano hayo mara ya kwanza.
Ndayiragije amesema:"Kila kitu kipo sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa leo ambao utakuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
"Kazi yetu ni kuona kwamba tunaanza vizuri kwenye mchezo wetu ili kufikia malengo ya kufanya vizuri mechi zetu ambazo tutacheza," .
Kila la kheri Stars
ReplyDelete