BEKI mpya wa kati wa klabu ya Yanga, Dickson Job amefunguka kuwa ameamua kuchagua jezi namba tano ndani ya klabu hiyo kama sehemu ya kumuenzi mtangulizi wake, Kelvin Yondani.
Job alikamilisha rasmi usajili wake wa kujiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili akitokea kikosi cha Mtibwa Sugar ya Morogoro, aliyoichezea kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.
Anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga kutokea Mtibwa Sugar msimu huu baada ya beki wa kulia, Kibwana Shomari aliyesajiliwa mwezi Agosti.
Job jana alikuwa sehemu ya
kikosi cha wachezaji wa Yanga walioingia kambini kuanza rasmi maandalizi ya
michezo ya mzunguko wa wa pili wa ligi inayotarajiwa kurejea mwezi Februari.
Akizungumzia kuhusu uamuzi wa kuchagua jezi namba tano,
Job alisema: “Kama mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa kati nimekuwa nikitumia muda
mwingi kujifunza kwa watangulizi wangu hasa Kelvin Yondani mchezaji ambaye
binafsi nampenda na nimekuwa nikimfuatilia na kujifunza vitu vingi kutoka kwake.
“Yondani amefanya
mambo makubwa akiwa na kikosi cha klabu za Simba na Yanga lakini pia akiwa na
jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivyo nami kama mchezaji mwenye
malengo ya kufanikiwa na kufika mbali ningependa kufuata nyayo zake na ndiyo
maana nimechagua jezi aliyokuwa akiivaa nikiamini naweza kuendeleza heshima
aliyoiacha.”
Chukua mazuri yake na yenye upungufu mwachie mwenyewe
ReplyDelete