PETER Muduhwa amejiunga rasmi na kikosi cha Simba leo Januari 26 anatarajiwa kutambulishwa Januari 27 kwenye Simba Super Cup.
Muduhwa amejiunga na Klabu ya Simba akitokea Klabu ya Higlanders FC ya Zimbabwe.
Nyota huyo ambaye ni beki amejiunga na Klabu ya Simba akitokea Cameroon ambapo timu ya Taifa ya Zimbabwe inashiriki michuano ya Chan.
Ikiwa nchini Cameroon, timu ya Taifa ya Zimbabwe imecheza jumla ya mechi tatu na haijaambulia ushindi ndani ya kundi A.
Imepoteza mechi zake zote tatu ikiwa inaburuza mkia na imefungwa jumla ya mabao matano huku safu yao ya ushambuliaji ikiwa imefunga bao moja.
Kinara ndani ya Kundi A ni Mali mwenye pointi 7 huku akifuatiwa na mwenyeji Cameroon mwenye pointi tano. Hivyo Zimbabwe haina chake kwa sasa ndani ya Chan baada ya kufangishiwa virago kutoka kwenye kundi ambalo linaonekana kuwa na ushindani mkubwa.
Paschal Serge Wawa ajiandae kisaikolojia
ReplyDeleteWawa umri umesogea, ndio maana anatafutiwa backup
ReplyDeleteNawatakia ushindi kamwe kwa wote snakubaguwA
ReplyDelete