January 26, 2021


 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake klabu ya Simba Queens wamezidi kuikaribia Yanga Princess baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 11-1 dhidi ya TSC Queens, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Simba MO Arena uliopo Bunju Jijini Dar es Salaam. 

Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 29 na kuwa nyuma kwa pointi mbili pekee dhidi ya vinara wa msimamo klabu ya Yanga Princess. 

Mchezo mwingine uliopigwa jana ni kati ya Ruvuma Queens na ES Unyanyembe ambao uliisha kwa Ruvuma Queens kuibuka na ushindi wa mabao 9-1.

 

1 COMMENTS:

  1. Tunashukuru kutuletea taarifa hii ya Soka la Wanawake Tanzania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic