KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa, kukosa umakini kwa washambuliaji wake katikati kutumia nafasi wanazotengeza uwanjani, ndiyo sababu kubwa ya kupata matokeo ya sare mfululizo katika michezo yao miwili iliyopita.
Yanga Jumamosi ilitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, sare hiyo ni ya pili mfululizo kwa Yanga kwenye Ligi Kuu Bara, ambapo waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.
Licha ya sare hiyo dhidi ya Mbeya City, Yanga imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo baada ya kujikusanyia pointi 45 katika michezo yao 19 waliyocheza mpaka sasa wakishinda mechi 13 na kutoa sare michezo sita.
Akizungumzia matokeo hayo Kaze amesema: “Imekuwa bahati mbaya sana kwetu kupoteza pointi nne katika michezo yetu miwili mfululizo iliyopita, hayakuwa malengo yetu na kwa maoni yangu nadhani tulipaswa kupata pointi sita katika michezo hiyo.
“Kwenye michezo yote miwili tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tukashindwa kuzitumia, nadhani tunapaswa kurekebisha hilo katika michezo yetu ijayo.
“Bado tuna malengo ya kupambania
ubingwa, na tutafanya kila jitihada kuhakikisha lengo hilo linatimia licha ya
ushindani mkubwa uliopo,”
Leo hajasema kuwa waamuzi ndio wanamfanya apate sare? Atakuwa katulia sasa.
ReplyDeleteAangalie asije akiingia kwenye mtego wa lawama kwa waamuzi badala ya kuganyia mapungufu ya Kikosi chake kama alivyokuwa Papa Zahera
ReplyDeleteHakukuwa na nafasi za wazi za kufunga dhidi ya mbeya city. Timu haikuwa tayari kwa mechi ya ushindani. Wanahitaji bado mechi za kutosha kurudi kwenye kiwango bora.
ReplyDeleteUsiwe na wasi. Engeneer hersi atatusaidia. Mechi zijazo ni kushinda mbele. Iwe bao la mkono marefa pesa hata makipa pesa. Mtakoma kama hamuijui yangs mwananchi
ReplyDelete