February 9, 2021

 


KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa ameridhishwa na maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakaopigwa siku ya Jumamosi.

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi na pointi zao 44 walizokusanya katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa wakishinda mechi 13 na kutoa sare kwenye michezo mitano.

Kuelekea mchezo huo Yanga imecheza michezo miwili ya kujipima nguvu ambapo imeshinda mchezo mmoja dhidi ya timu yao ya vijana U20, na kupoteza mchezo mmoja mbele ya African Sports.

Akizungumzia maandalizi hayo, Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema baada ya kucheza michezo miwili ya kirafiki, kocha wa klabu hiyo Cedric Kaze ameridhishwa na maendeleo ya nyota wake.

“Kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa siku ya Jumamosi, kocha Kaze anaonekana kuridhishwa na viwango vya nyota wake baada ya wiki mbili za mazoezi tangu tulivyoanza rasmi kambi Januari 25.

“Tunajua mchezo dhidi ya Mbeya City utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunafanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo, tumepata michezo ya kirafiki ambayo imempa kocha mwanga wa wapi tumeimarika na wapi bado tunaonekana kuwa na mapungufu,”

5 COMMENTS:

  1. Msitie wasiwasi Mbeya City ni miongoni mwa timu zipo katika hatihati

    ReplyDelete
  2. Tulistahili kupata mechi kama mbili zaidi za kirafiki. Timu haijarudi mahali pake.

    ReplyDelete
  3. Kwakikosi kilichopo kinatosha kuiangamiza kabisa mbeya city

    ReplyDelete
  4. so tuamin tutashinda ! maana Tim ambazo zinapigania zisishuke huwa ngum sana kuzifunga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic