February 9, 2021

 


KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, klabu ya Simba tayari kimewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, kwa ajili ya kuanza safari yao ya kwenda nchini DR Congo kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.

Simba inatarajiwa kuivaa Vita katika mchezo wa kwanza wa kundi A unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Stade des Martyrs, uliopo Kinshasa nchini Congo majira ya saa 11 jioni kwa saa za DR Congo ambayo ni sawa na saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki mchezo utakaopigwa siku ya Ijumaa Februari 12, mwaka huu.

Simba iliondoka jana saa 10 jioni uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar ikiwa na wachezaji wake wote mahiri akiwemo kiungo Jonas Mkude.


 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic