February 9, 2021

 

 


KOCHA msaidizi wa klabu ya Azam, Vivier Bahati amesema kuwa anaamini kikosi chake kilistahili kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa kiporo uliopigwa Jumapili iliyopita dhidi ya wapinzani wao Simba.

Katika mchezo huo ulioisha kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2, Azam walionyesha kiwango kizuri hasa katika kipindi cha pili baada ya kuingia kwa Yahya Zayd na Mudathir Yahya ambapo walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia.

Kwenye mchezo huo mabao ya Azam yalifungwa na Idd Selemani Nado na Ayoub Lyanga, huku Simba wao wakipata mabao yao kupitia kwa Meddie Kagere na Luis Miquissone. Sare hiyo inaifanya Azam sasa ifikishe michezo minne bila kupata ushindi mbele ya Simba. 

Bahati a
mesema kama washambuliaji wake wangekuwa makini kutumia nafasi walizotengeneza basi wangefanikiwa kuibuka na ushindi.

“Ulikuwa mchezo mzuri na wa ushindani, wapinzani wetu walikuwa na mchezo mzuri ndani ya kipindi cha kwanza wakitawala mchezo na kutengeneza nafasi, lakini tulivyokwenda mapumziko tuliongea na vijana wetu na kurekebisha makosa tuliyofanya.

“Na kila mmoja aliona jinsi tulivyocheza kipindi cha pili tuliweza kutawala na kutengeneza nafasi nyingi zaidi na kama washambuliaji wetu wangekuwa na utulivu wa kutumia nafasi tulizotengeneza basi nina uhakika tulikuwa tunastahili kuibuka na ushindi dhidi ya Simba,”

Sare hiyo imeifanya Azam sasa kufikisha pointi 33 zinazoendelea kuwaweka kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 18.

 

 

 

 

10 COMMENTS:

  1. Hizi nazo porojo,labda Mimi Kiswahili sijui kustahili ni pale unapokuwa Bora zaidi ya mwenzio ,hapa Azam Kama ni ninyi mnaosoma hivyo inaonekana hamjakomaa Kisoka Takwimu za mchezo haziwapi ushindi,hata hicho kipindi Cha pili mnachojivuna nacho Mimi Kama Mwananchi sioni Kama mlistahili hamkuwapa shinikizo mno Simba, nadhani walibweteka wakijua always wanawafunga ndipo mkapata hizo Chances pengine na udhaifu wa defence yao bt in reality wali wa command mno kipindi chote Cha mchezo ule.

    ReplyDelete
  2. Hawa ni azam au waandishi uchwara wa utopolo? Wanaongea bila takwimu? Tifanye azam basi walishinda, sisi timeshasahau huo mchezo tuko kimataifa sasa, endeleeni na utopolo wenu

    ReplyDelete
  3. Sasa kwa nini hamkushinda?

    ReplyDelete
  4. Hahaha ukweli uko wazi hata kama mhamupendi kusikia nyie miungu watu msiopenda timu yenu kusemwa ila majibu munayo wenyewee

    ReplyDelete
  5. Anasema anaamini kuwa kikosi chakeke kilistahiki kupata ushindi dhidi ya Simba Kwani alighafilika kuwa mbali ya kukosa peneti Mnyama alikosa magoli mane ya wazi kabisa na katika kipindi cha kwanza Mnyama alimiliki mpira karibu 80%? Anachekesha jamaa

    ReplyDelete
  6. Nguruwe fc mlisitahili kupigwa kabisa maana mlisawazisha mapaka fc nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mapaka FC wana kelele... kwani aliyesawazisha ni nani?

      Delete
  7. Manyani Fc aka utopolo wa vidimbwini wanafurahia sare ya Azam baada ya kupigwa kidude na wa wamchangani African sport.

    ReplyDelete
  8. اHao ni kama kuku mpige teke halafu mrushie machicha atakuwa keshasahau na kurejea ni wepesi kusahau na ile kuchapwa na timu ya chini ya minazi zamani wameshasahau eti wanamcheka Mnyama ambae yupo katika hesabu za Africa kwa kikosi bora na hivi wapo Congo wakiutaka ubingwa wa Africa.

    ReplyDelete
  9. Kawahoji tena kama na leo walistahili kushinda dhidi ya coastal

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic