February 20, 2021

 


HASSAN Kabunda, nyota wa KMC leo Februari 20 amepachika mabao mawili wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. 

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo KMC yenye sera ya pira spana imeifunika ile sera ya pira burudani ya Kagera Sugar.

Kabunda ambaye ni winga mzawa alipachika mabao hayo dakika ya 78 na 88 huku lile la ufunguzi likifungwa na Abdul Hilallary dakika ya 16.

Kwa msimu wa 2020/21 timu hizi zimegawana pointi tatutatu ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar ilishinda kwa bao 1-0 lilipachikwa na Yusuph Mhilu.

Leo imekuwa zamu ya KMC kusepana pointi tatu na imefunga mabao matatu ikiwa nyumbani.

Mchezo uliopita kwenye ligi kwa KMC ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC huku Kagera Sugar ikiwa imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Yanga.

4 COMMENTS:

  1. Hao walishamaliza ligi walipotoka sare na mabingwa wa ukweli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bingwa wa kweli ni yule amabaye hata akienda kimataifa anafanya vizur

      Delete
  2. Makocha na wachezaji wa Kitanzania wakicheza na YANGA /Simba wamemaliza Ligi

    ReplyDelete
  3. Mpira una matokeo ya aina tatu sare,kufungwa na kufunga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic