February 20, 2021

 


BAADA ya kupata matokeo ya sare tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu soka Tanzania Bara, kikosi cha klabu ya Yanga kimewaahidi mashabiki wake kutorudia makosa hayo huku mastaa wao wakila kiapo cha kupambana.

Yanga Jumatano iliyopita walipata matokeo ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi uliopigwa katika dimba la Mkapa jijini Dar, hivyo kufikisha sare ya tatu mfululizo huku wakiwa hawajashinda mchezo wowote wa ligi tangu Desemba 23, walipoifunga ihefu mabao 3-0.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar nahodha wa kikosi cha klabu ya Yanga Lamine Moro amesema: “Tumepata matokeo ya kukatisha tamaa kwenye michezo mitatu iliyopita, kwa upande wangu naamini tulipambana lakini hatukuwa na bahati.

“Niwaombe mashabiki wetu watuunge mkono, sote tunajua ni kwa jinsi gani tumeumia, lakini bado tunapaswa kushikamana na kuendelea kupambana kama familia moja.

"Tunawaahidi mashabiki wetu kuwa leo tutawarudishia tabasamu kwenye nyuso zao,”

 


4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic