February 19, 2021



CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaoochezwa kesho, Uwanja wa Uhuru.

KMC inashuka Uwanja wa Uhuru kuwakabili Kagera Sugar ikiwa imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC, Uwanja wa Uhuru.

Inakutana na Kagera Sugar ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo utachezwa majira ya 8:00 mchana na kwa sasa KMC ipo kwenye maandalizi ya mwisho kama ilivyo kwa Kagera Sugar.

Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Kaitaba, KMC iliacha pointi zote tatu baada ya kufungwa bao 1-0 ambalo lilipachikwa na Yusuph Mhilu.


Christina amesema:“ Tunahitaji kushinda mchezo wetu wa kesho, ushindi ni mkakati wetu wa kwanza, tunajua duru hii ni ngumu kwa sababu kila timu inahitaji alama tatu muhimu.

"Kikubwa tunaendelea kujituma katika maandalizi yetu kila mchezo kwetu ni fainali lengo ni kuhakikisha kwamba kwenye mchezo huo tunakwenda kupata alama tatu.




2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic