February 19, 2021



UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly, Waarabu wa Misri, watatumia kauli mbinu ya TOTAL WAR: POINT OF NO RETURN.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo chanya kwa kuwa wamekuwa wakifanya vizuri Uwanja wa Mkapa.

Mchzo huo ambao umeshika hisia za mashabiki wengi unatarajiwa kuchezwa Febbruari 23 tayari kikosi kimeanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo mgumu.

 “Mabingwa wa Afrika Al Ahly ambao wametoka kushiriki ubingwa wa dunia na kushika nafasi ya tatu watakuja kuwakabili mabingwa mara nyingi zaidi wa Afrika Mashariki ambao ni Simba.

"Rekodi hizo zitaufanya mchezo kuwa wa kipekee ndani ya uwanja na kila mmoja ninatambua kwamba anajua namna ambavyo tunahitaji ushindi.”

"Mara ya mwisho tulikutana hapa Dar tukawafunga  1-0 kwenye mechi tuliyosema "YES WE CAN" na tukaweza na mara zote tukicheza Tanzania tunawafunga.

“Al Ahly sio timu nyepesi. Tunaposema tunaweza kuwafunga tunajua ukubwa wao, lakini Simba hupenda mechi kubwa kama hizi.

"Mechi ya mwisho tuliita WAR IN DAR, mechi ya jasho na damu ndani ya dakika 90 na sasa tunasema TOTAL WAR : POINT OF NO RETURN hii sasa ni vita kamili ya ndani ya uwanja,".


3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic