KOCHA mkuu wa Azam, George Lwandamina amefunguka kuwa ubovu wa miundombinu ya viwanja hapa nchini unachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mchezo wa soka.
Azam ambayo haijapata ushindi tangu Desema 31, mwaka jana, juzi Alhamisi, ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Coastal Union mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Akizungumzia sababu ya matokeo yasiyoridhisha kwenye kikosi chake kocha Lwandamina amesema
kuwa ubovu wa
viwanja ni changamoto kubwa inayosababisha timu nyingi kushindwa kucheza mpira wa burudani au soka la pasi.
“Miundombinu ya viwanja kwenye mchezo wa soka ni miongoni mwa vitu vya muhimu katika ukuaji wa mchezo huu duniani.
"Hii ni kwa sababu ili uweze kucheza mpira wa pasi nyingi, na burudani unahitaji mazingira ya uwanja unaoruhusu hali hiyo, kama itashindikana basi unakuwa kwenye wakati mgumu.
"Kwa mfano sisi Alhamisi tulipoteza mchezo wetu dhidi ya Coastal, matokeo ambayo yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa uwanja wa Mkwakwani ambao ulishindwa kuturuhusu kucheza mpira wa pasi za chini.
asante mwandishi kwa kuzinduka muda mfupi baada ya wadau kulalamika kuwa kwa desturi Yanga ikishinda mnaandika habari nyingi za uchambuzi wa mechi na kuweka msimamo wa ligi...leo yamepita masaa manne baada ya mechi ya Mbeya city na Yanga..ni habari ya Namungo tu ndiyo mlichapisha..
ReplyDeleteje hakukuw hata na ligi inachezwa ulaya.
poleni goli la kubaka na dhuruma la Kaseke haikuwa ridhiki...matamania hawajatokea vile..maisha yanaendelea...jipoeni moyo na endeleeni kuandika
tuandikie na kocha Kaze ameliaje na penalti halali ya Mbeya city..pale kilicho kuwa haramu na la kubaka ni goli ambalo halijavuka msitari..basi hata huyo refa angeamua iwe kona kama ilivyokuwa mwaka juzi wakati kipa yanga karudisha na kuubania mpira kwenye mlingoti..
ReplyDeleteMlifurahi alipominya penalt yetu.. tusubiri ilimradi midomo isije kwenda upande
Delete