February 23, 2021


 KOCHA Mkuu wa Al Ahly ya Misri amesema kuwa anawatambua vema wapinzani wake Simba kwa kuwa amewafuatilia kwa muda mrefu ikiwa ni kwenye mechi zao za nyuma pamoja na ile waliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita,DR Congo.

Leo Uwanja wa Mkapa kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kimataifa katika Ligi ya Mabingwa na Afrika huku kwenye upande wa Kombe la Shirikisho ni Namungo FC.

Pitso Mosimane amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao anatambua ni imara ndani ya Simba ni pamoja na kiungo Clatous Chama, Luis Miquissone,Rarry Bwalya na Taddeo Lwanga.

Kocha huyo amesema:"Kuna wachezaji wazuri na tunatambua kwamba tunacheza na wachezaji wa aina gani kwa kuwa tumewafuatilia kwa muda na tunatambua namna ya kuwazuia hawawezi kutupa shida ndani ya uwanja.

"Hatuna hofu tutaingia ndani ya uwanja tukiamini kwamba kuna kitu ambacho tunakihitaji nao ni ushindi hakuna jambo jingine,".

1 COMMENTS:

  1. Mi nataka kutoa povu kwa waandishi wetu wa habari linapokuja suala la press conference na makocha wageni,Yaani kwangu mimi naona kama vile ulimbukemi umezidi kwa wanahabari wetu kulazimisha kuuliza maswali kwa kiengereza yaani inatia kichefuchefu na ni aibu na janga la taifa.Hili Taifa limekuwa kama halina mwenyewe.waandishi hawa ni watanzania wapo kwenye ardhi ya Tanzania wamiliki wa Lugha tamu yenye ladha ya kipekee dunian lakini wale watu wenye jukumu la kuitangaza Lugha yetu ndio wanaokigaraza kiswahili.Nina uhakika hata Mosmane kocha Wa Ahly alikuwa anakereka na kushangaa kuona kuwa wawakilishi wakazi wa Lugha inayopigiwa kampeni kuwa lugha ya Waafrica wanaikana Lugha yao kwenye ardhi yao na medani ya kimataifa whata shame? Wewe unadhani wale warabu waliomuuliza maswali kwa kiarabu Mosmane hawajui kiengereza? We muandishi upo nyumbani kwako twanga tu kiswahili jimwage kazi kwake mgeni mpe kazi ya kutafakari mgeni nini kimeongewa tunao wataalam wengi tu wa lugha za kigeni wa kudadavua maswali kwa ufasaha na madaha yanayotakikana. Lazima tujivunie kiswahili chetu naona kuna tatizo kwenye tasnia ya habari kwa kiasi kikubwa kama watu waliotarajiwa kuwa namba moja kukitangaza kisheahili lakini ndio wanaokampeni kukipiga vita kiswahili kwa kweli hii sio sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic