February 28, 2021


 KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa rekodi za wachezaji alizopewa na makocha wa timu zao pamoja na maoni ya makocha yamempa nafasi ya kuteua kikosi hicho.


Miongoni mwa majina ambayo yalimvutia ni pamoja na mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi ambaye yupo chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze akiwa amehusika kwenye pasi mbili za mabao.


Yanga imetoa jumla ya wachezaji nane kikosi cha Stars ambapo wamehusika kwenye mabao 14 kati ya 34 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.


Mbali na huyo kutoka Yanga pia yupo kipa namba moja Metacha Mnata, Bakari Nondo Mwamnyeto yeye ni beki wa kati ametupia bao moja ndani ya ligi ingizo jipya ndani ya Yanga, Dickson Job ni beki wa kati ila majeraha yamemfanya awe nje.


 Yassin Mustapha yeye ni beki wa pembeni, Feisal Salum ‘Fei Toto’, yeye ni kiungo mkabaji ametupia bao moja. Farid Mussa yeye ni kiungo mshambuliaji ametoa jumla ya pasi tatu za mabao.


 Deus kaseke yeye ni kiungo ndani ya kikosi cha Yanga ametupia mabao sita na pasi moja. Nyota hao wameitwa Stars kwa ajili ya kikosi kitakachoingia kambini Machi 8 ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Afcon.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic