February 7, 2021

 


LEO Februari 7, Simba imepata Mwenyekiti mpya ambaye anakuwa mrithi wa mikoba ya Sued Mkwabi ambaye alibwaga manyanga Septemba 2019.

Uchaguzi wa leo ambao umefanywa na Wanachama waliokidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya uanachama umefanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba ni Murtaza Mangungu baada ya kupata kura 802 (70.35%) akimshinda Juma Nkamia aliyepata kura 330 (28.95%).

Jumla ya kura zilizopigwa ni 1140 na kura 8 (0.7%) zimeharibika.

5 COMMENTS:

  1. Mwenyekiti Anza na Viporo Vimeanza kuchacha

    ReplyDelete
  2. Kidimbwi FC wanafurahia kuongoza ligi teh teh teh , alafu ligi yenyewe bado mechi karibu 17 round ya pili hii Kuna timu zinakwepa kushuka daraja alafu mtegemee huo ushindi wa kigoli kimoja naona muda si mrefu utasikia TFF ni simba

    ReplyDelete
  3. Idd Suleiman "NADO"

    ReplyDelete
  4. Ili Simba iweze kuwa imeongoza Ligi Round ya kwanza ya Ligi njia pekee ni kuiingiza kwenye msimamo Mechi ya Kirafiki Kati ya Yanga na African Sports

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic