BAADA ya kurejea kutokea nchini Angola, Uongozi wa kikosi cha klabu ya soka ya Namungo umefunguka kuwa yale yote ambayo wamekutana nayo katika safari hiyo, yamewapa funzo na hamasa ya kuhakikisha wanajiandaa vizuri na hawarudii makosa kuelekea michezo yao ya kimataifa.
Namungo ilirejea nchini juzi usiku kutokea Angola ilipokwenda kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Clube Desportivo 1º de Agosto ambao hapo awali ulipangwa kufanyika siku ya Jumapili.
Wakiwa nchini Angola, Namungo walikumbabna na matukio mengi ikiwemo wachezaji wake watatu ambao ni Lucas Kikoti, Hamis Mgunya, Fredi Tangaru na Ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa klabu, Omary Kaaya kutajwa na mamlaka ya afya za Angola kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, huku viongozi wa Namungo wakitafsiri matukio hayo kama uhalifu wa kupanga uliofanywa kwa lengo la kuwadhoofisha.
Sakata hilo lilipelekea mchezo huo kufutwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF), huku kamati maalum ikikaa kulijadili suala hilo, na kufikia muafaka wa michezo hiyo yote miwili kupigwa nchini Tanzania.
Juhudi za Namungo kurejea nyumbani na nyota wake wote ziligonga mwamba na kulazimika kuwaacha wale waliotajwa kuwa na Corona mpaka pale watakapopona.
Akizungumzia yale ambayo kikosi chao kimekutana nayo, Ofisa habari wa Namungo, Kindamba Namlia alisema: “Timu imerejea salama nchini bila wachezaji wake watatu na kiongozi mmoja ambao kimsingi kutokana na sheria za mamlaka ya afya wao wataendelea kubaki.
“Wachezaji hao ambao ni Kikoti, Mgunya, Tangaru pamoja na Ofisa mtendaji mkuu (CEO) wa klabu, Omary Kaaya watasalia kutokana na mamlaka zao kusema wana ugonjwa wa COVID-19, na wataruhusiwa kutoka Angola kama tu watapimwa na kugundulika hawana maambukizi.
“Yote yaliyotokea yametupa funzo, hivyo tutajipanga vizuri
zaidi kuelekea michezo yetu ijayo ya kimataifa,”
0 COMMENTS:
Post a Comment