GUU la Michael Sarpong, mshambuliaji wa Yanga,inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze limekwama Uwanja wa Mkapa kwa muda wa dakika 426 bila kucheka na nyavu.
Bao la kwanza Sarpong aliwafunga Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, bao la pili aliwatungua Biashara United, Uwanja wa Karume. Bao tatu aliwatungua Simba kwa mkwaju wa penalti, Uwanja wa Mkapa.
Bao la nne aliwatungua Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Desemba 6.
Baada ya hapo amecheza jumla ya mechi sita ndani ya ligi zote hajafunga zaidi ya kutoa pasi moja za mabao. Hivyo mshambuliaji huyo amehusika kwenye mabao matano kati ya 33 yaliyofungwa na timu hiyo akiwa amefunga manne na pasi moja ya bao.
Hizi hapa za kwenye ligi:-Mwadui 0-5 Yanga alitumia dakika 90,Yanga 3-1 Dodoma Jiji alitumia dakika 45,Tanzania Prisons 1-1 Yanga alitumia dakika 90,Mbeya City 1-1 Yanga alitumia dakika 90,Yanga 3-3 Kagera Sugar alitumia dakika 45, Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa dakika 66.
Sarpong amesema kuwa anaamini mashabiki wanahitaji kuona akifunga jambo ambalo analipambania na atafanya hivyo kwenye mechi zake zijazo.
Huyu Yanga walikuwa wakimwita mashine ya magoli hatari sana Kumbe ni maovu ya sabuni na huku mamilioni keshayatia mfukoni
ReplyDelete