February 26, 2021


 LICHA ya mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Simba, Meddie Kagere kukosa penalti dakika ya 20 haikuzuia timu hiyo kushinda mbele ya African Lyon, Uwanja wa Mkapa.

Kagere mwenye mabao 9 ndani ya ligi, alipiga pembeni kidogo ya lango ambalo lilikuwa linalindwa na Bwanaheri Abdalah ambaye aliweza kuwa imara licha ya kuokota nyavuni mabao 3-0 ambapo mawili aliyasbababisha mwenyewe huku moja ikiwa ni uzembe wa mabeki.

Mabao ya Simba yalifungwa na Ibarahim Ajibu dakika ya 9 baada ya Bwanaheri kupangua kona na ikakutana na kichwa cha Ajibu. Kagere alikuwa na nafasi ya kuongeza bao la pili dakika ya 20 baada ya Perfect Chikwende kuchezewa faulo ndani ya 18 ila alikwama.

Iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 43 kupachika bao la pili ambalo lilifungwa na Ajibu tena na kuwafanya waende mapumziko wakiongoza kwa mabao 2-0.

Jitihada za African Lyon kipindi cha pili kuzuia mashambulizi zilikomea dakika ya 63 baada ya Chikwende kupachika bao la tatu na ukawa msumari wa mwisho.

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa wachezaji wake walijituma jambo lililowapa matokeo chanya.

Kwa ushindi huo wanatinga hatua ya 16 bora wakiwa ni mabingwa watetezi wa taji hilo la Shirikisho na mchezo wao ujao ni dhidi ya Kagera Sugar ya Mecky Maxime.

5 COMMENTS:

  1. Utopolo wamesarenda. Wako ndembwe ndenbwe.Wanajua sasa ndio muda wa kutafuta visingizio.
    Naiona 4G ingine kwa mbali.

    ReplyDelete
  2. refa kashasema hata ukiwa mbele yang na una mpira nkikusukuma ni bega kwa bega haijalishi ni mtu wa mwisho

    ReplyDelete
  3. Utopolo naona siku hizi kimya kimetanda ni kama vile kimya cha alieishiwa na nguvu na kukata tamaa. Nawausia kuwa Kuanguka sio kushindwa, kushindwa ni pale unaposhindwa kunyanyuka tena na vilevile hakuna furaha ya ushindi kama hujaonja machunngu ya kushindwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic