UONGOZI wa Klabu ya Yanga, inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze umewapa pongezi nyoa wake wawili kwa kuitwa kwenye timu zao za taifa.
Nyota hao wa kigeni wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu hiyo inayoongoza Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.
Ikiwa tayari imecheza jumla ya mechi 21 na imekusanya pointi 49 na haijapoteza mchezo hata mmoja ndani ya ligi zaidi ya kushinda mechi 14 na sare 7.
Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram wa Yanga ulitoa pongezi kwa kiungo Mukoko Tonombe ambaye ameitwa timu ya taifa ya Congo pamoja na kiungo mshambuliaji Said Ntibanzokiza ambaye ameitwa timu ya taifa ya Burundi.
Wameitwa kwenye timu zao za taifa ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu michuano ya Afcon. Hata Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen leo Februari 26 ametangaza kikosi cha timu ya taifa kinachotarajiwa kuingia kambini Machi 8.
Hongera sana Yanga sio kwa kwakuwa hawajafungwa hata mara moja katika michezo ya ligi lakini wachezaji wao wawili wamechaguliwa katika timu zao za taifa kama walivotangaza wenyewe
ReplyDeleteHao 2 ni wa Kimataifa walioitwa. Ila wazawa wapo 8. Jumla wapo 10
DeleteSEMA HAWAJAPOTEZA MCHEZO, ILA KUFUNGWA WAMFEUNGWA NA WANAONGOZA MECHI PIA
DeleteKwenye table lose inaonyesha 1?
DeleteNyie msifungwe toeni tu sare mwisho wa siku bingwa anawazidi na pointi kibao
ReplyDeleteKutokupoteza mchezo ni heshima na Credit kubwa, sio kila team inaweza
ReplyDeleteWazee wa sare hongereni sana hio inatokana na ulinzi kuelekea kutokufungwa mashine na mashine za mabao kibao. Hongereni sana na vilevile ikiwa hamkukubali kufungwa pia msikubali Manara kubeza yanga
ReplyDeleteSimba ya Patrick Phiri, iliwahi kuchukua ubingwa bila kufungwa, ingawa waliPata matokeo ya sare kama yanga. Yanga wasijione ndiyo wa kwanza kuandika historia ya kuwa na mechi hawajafungwa.
ReplyDeletekama ambavyo nanyi msipige kelele sana na kujiona wa kwanza kumfunga al ahly ambae ni bingwa mtetezi wa klabu bingwa afrika......hata yanga walishawahi kumfunga al ahly mwaka 2014 akiwa bingwa mtetezi.
DeleteBaelezi Bamikia
Delete