March 16, 2021

 


IMERIPOTIWA kuwa wachezaji 8 wa kikosi cha Al Merrikh ya Sudan ambayo leo Machi 16 itacheza na Klabu ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wamekutwa na Virusi vya Corona. 

Kupitia ukurasa rasmi wa Istagram wa Al Merrikh umeripoti kuwa wanaamini ni mpango wa kuwadhoofisha ambao umechezwa jambo ambalo limewafanya wapeleke file hilo mbele Umoja wa Afrika, (AU).  

Taarifa zinaeleza kuwa wamepewa matokeo hayo saa moja kabla ya mchezo wa leo ambao unachezwa Uwanja wa Mkapa.


Miongoni mwa wachezaji ambao wametajwa kuwa na Corona ni Abdul Rahman Karngou, Altaj Yaqoub, Bhakit Khamis, Ramadan Ajab, Tony, Bakir Al Madina, Saif Al-Damazin, Emad Abdul-Manim.

15 COMMENTS:

  1. Hili mbona limekaa vibaya, wachezaji 8? Hebu tuwe serious basi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lkn CAFwana watu wao.Pia ukumbuke hata kwao kabla ya mechi pale Sudan kuna wachezaji wao 5 walikutwa na corona.

      Delete
    2. Almerekh wamesahau walivyowafanyia wagana?

      Delete
  2. Ndio mpira wa Africa figisu mwanzo mwisho, kisha watu wanajisifu wanakikosi kipana

    ReplyDelete
  3. Huo ni uongo haiwezekani wachezaji wote hao wakutwe na Corona mwandishi umetudanganya.

    ReplyDelete
  4. Saleh jembe acha unafiki...hizi sio habari za kuchapisha kama wewe ni mzalendo..

    ReplyDelete
  5. Shida ya huyu mwandishi ni yanga.Hivi sasa anaumia sana anavoona simba anaongoza

    ReplyDelete
  6. Hawa walishaanza kuumwa tangu kwao. Sasa kama kwao tu wachezaji watano walikutwa na corona, kwani ni ajabu kusikia wamewaambukiza wengine watatu?

    ReplyDelete
  7. Matopolo yamekereka na wala hawawezi kujizuia au angalau kuona aibu. Wenye roho za mbaya kama hizo vipi wataraji mafanikio na hio ndio sababu ya mikosi isiyoisha.
    Masikini leo hawapati usingizi

    ReplyDelete
  8. Jee walipochapwa nne na Vita baadae tau na Al Ahli na kutolewa kwao kwa kugundulikana na corona huko pia walipeleka faili Caff

    ReplyDelete
  9. Replies
    1. Bado mnateseka na Platinum? Watu tulishasahau tunawaza AS Vita kwa Mkapa. Kwanza sio Simba wanaopima corona, kuna maafisa wa CAF wanasimamia zoezi hilo. Hata sisi tulipoenda Congo, wachezaji wanne na kiongozi mmoja walizuiwa kwa corona.Ujanja ni kutumia fursa ya CAF ya kusajili wachezaji 10 zaidi, kama hawakusajili ni juu yao

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic