March 21, 2021


MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msola amesema kuwa kuondoka kwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ni pengo kubwa kwa Afrika na Tanzania kiujumla.

Msolla amesema kuwa Magufuli alikuwa ni mpenda michezo na furaha yake ilikuwa ni kuona matokeo chanya jambo ambalo linakuwa ni kazi kwa wanamichezo kupambana kufanya vizuri.

"Magufuli alikuwa ni mpenda michezo na alikuwa anapenda kuona timu zote zinapata mafanikio na kuondoka kwake ni pigo kwa kila Mtanzania na ni pengo kubwa.

"Ni vyema tuseme kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya kwa sasa kwa ajili ya kumuenzi Magufuli kwa kuwa ni mipango ya Mungu," amesema.

Leo viongozi wa Yanga pamoja na wachezaji watajitokeza Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa Magufuli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic