March 2, 2021


 STRAIKA raia wa Burundi, Alex Kitenge ambaye aliwahi kucheza Ligi Kuu Bara misimu miwili iliyopita akiwa na Stand United, amemuomba kocha wa Yanga, Cedric Kaze kumpa nafasi kwenye timu hiyo hata ikilazimika kufanya majaribio kwanza.

 

 Kitenge, aliyefunga mabao matatu msimu huo wa 2018-19, alifunguka kuwa anatamani kurejea tena Tanzania kucheza soka na timu ambayo anaipa kipaumbele ni Yanga kwa sababu ina wachezaji wazuri akiwemo Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ambaye aliwahi kucheza naye soka mitaa ya Bujumbura.

 

 

Kitenge kwa sasa anakipiga kwenye Klabu ya Atletico inayoshiriki Ligi Kuu Burundi na mchezo wake wa kwanza alifunga bao dhidi ya Vital’o na kuipa pointi tatu timu hiyo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Umoja.

 

 

 Kitenge amesema: “Natamani kurudi Tanzania kucheza tena soka na timu ambayo naitazama ni Yanga.

 

 

"Nimejaribu kuwasiliana na kocha wao Kaze lakini bado sijapata mrejesho mzuri, mimi naomba anipe japo nafasi ya kufanya majaribio ili nimuonyeshe uwezo wangu wa kufunga mabao.”

 

 

Alipotafutwa Kaze juu ya suala hilo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa meseji hakukuwa na majibu. Kitenge aliwahi kupata jina akiwa Stand United, baada ya kuwafunga Yanga hat-trick kwenye mchezo uliochezwa Septemba 16, 2018 kwenye Uwanja wa Mkapa zamani Taifa na mechi ikienda dakika 90 kwa Yanga kushinda 4-3, ikiwa chini ya kocha mkongo Mwinyi Zahera.


Chanzo: Championi

4 COMMENTS:

  1. Haya utopolo mtambo wa mabao huo

    ReplyDelete
  2. Pumbavu kabisa!!! Yaani wameshaona wana fursa ya kuanzisha kijiji cha Warundi Jangwani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ukabila wewe, mtambo wa mabao huo tinauhitaji uje utupigie mnyama

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic