BAADA ya kusikia kifo cha aliyekuwa Rais wa
Tanzania John Magufuli, kiungo wa kati wa Klabu ya AS Vita, Jeremy Mumbere
amemlilia rais huyo huku akisema kuwa yeye alikuwa ni kati ya shabiki mkubwa wa
kiongozi huyo.
Jeremy Mumbere
kwa sasa ni nahodha wa kikosi cha AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo.
Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja
kutoka nchini DR Congo, Mumbere alisema kuwa amesikitishwa kusikia taarifa za
kifo cha Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kwani alikuwa ni kiongozi mzuri
ambaye alikuwa akimfuatilia kwa ukaribu kutokana na utendaji wake kuwa mzuri
jambo ambalo lilimfanya awe anamfuatilia mara kwa mara.
“Nimesikitika sana kusikia taarifa za msiba wa
Rais wa Tanzania, John Magufuli ni moja kati ya rais bora kuwahi kutokea katika
bara hili la Afrika, alikuwa ni kiongozi anayependa maendeleo na Tanzania
ilikuwa imepata mengi mazuri kutoka kwake.
“Utendaji wake wa kazi ulinifanya niwe shabiki
yake kwa kumfuatilia kwa mambo mengi, hakika Tanzania imempoteza mtu wa muhimu
sana kwani hata huku DRC tulikuwa tunampenda sana Rais Magufuli,” alisema kiungo
huyo.
Naye mwenyekiti wa mashabiki wa Klabu ya TP
Mazembe, Jean Mazembe Kazadi alisema: “Niwape pole Watanzania wote na Afrika
kwa jumla kwa kumpoteza Rais Magufuli, nasema Afrika kwa jumla kwa kuwa ndiye
alikuwa kioo kwa viongozi wengi hapa Afrika katika maamuzi ambayo wengi
walikuwa hawezi kasoro yeye ambaye alikuwa akithubutu, wote tumuombee
Magufuli,” alisema kiongozi huyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment