March 25, 2021


 DAVID Alaba mwenye miaka 28 anatajwa kujiunga na Klabu ya Real Madrid baada ya kupewa ofa ya pauni 165,000 sawa na shilingi milioni 528 kuwa ni mshahara wake kwa wiki mbali na marupurupu ya kutosha.

Beki huyo wa Klabu ya Bayern Munich raia wa Austria atasepa ndani ya klabu hiyo pale msimu huu utakapomeguka na amekubali kujiunga na vigogo hao wa Hispania.

Kwa mujibu wa ABC Deportes Alaba amekubali kwa mdomo kujiunga na Real Madrid kufuatia ofa kubwa ambayo imewekwa mezani na mabingwa hao mara 13 wa Ulaya.

Alaba anatazamwa kuwa mbadala wa Sergio Ramos ambaye imekuwa ikielezwa kuwa anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic